Klabu ya Tottenham Hotspur imeonesha nia ya kuzima ndoto za Real Madrid na Paris Seint German (PSG), timu ambazo zinamtaka kocha wao Mauricio Ponchettino.

Klabu hiyo inajipanga kumpa kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 mkataba mpya utakao kuwa na thamani ya Euro million 5.8 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Telegraph, Spurs imedhamilia kumfanya kocha huyo raia wa Argentina kuwa kocha anayelipwa vizuri Zaidi katika ligi kuu nchini Uingereza.

Aidha, baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo akiwemo Delle Alli, Harry Kane, Jan Vertonghen, Hugo Lloris na Christian Eriksen nao wanatajwa kunufaika na mkataba mpya utakaowafanya kuwa moja kati ya wachezaji wanolipwa pesa nyingi ndani ya EPL.

Ponchettino ambaye ameifundisha Tottenham kwa miaka 4 mpaka sasa amekuwa akizivutia timu nyingi barani ulaya kufuatia kufanya vizuri ndani ya klabu hiyo.

Magufuli aishukia Tanesco, aagiza kushusha bei ya umeme
Juma Nature, Marlow, Mandojo wamuumiza kichwa Ray C

Comments

comments