Serikali imesema, haina malengo ya kutoza Wananchi wake kodi au tozo kwa ajili ya kuwapa mzigo, bali inalenga kuwahusisha Watanzania wote kwa umoja wao katika juhudi za kujikwamua kimaendeleo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba Bungeni jijini Dodoma hii leo Septemba 20, 2022 na kudai kuwa kulikuwepo na hali mbaya ya barabara za vijijini zilizokosa matengenezo kwa ufinyu wa bajeti, kadhalika, tulikuwa na vijiji ambavyo havijawahi kuwa na barabara ya aina yeyote tangu nchi ilipopata uhuru.

Amesema, “Akina mama wajawazito walikuwa wakibebwa kwa vitanda kupelekwa hospitali na wengine kupoteza maisha njiani, watoto wa shule wakibebwa na maji kwa vijito tu kukosekana kwa madaraja huku kukiwepo na kilio kikubwa cha ukosefu wa vituo vya afya vya kisasa vijijini na wagonjwa wote walikuwa wanalazimika kutegemea hospitali za wilaya tu.”

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.

Dkt. Mwigulu ameongeza kuwa, “Maeneno mengine hata hospitali za wilaya hazikuwepo, sehemu nyingine wananchi walilazimika kwenda hospitali za mikoa jirani, tulikuwa tunapoteza maisha ya watanzania kutokana na umbali wa kufuata huduma za afya na tulikuwa na kilio kikubwa cha uwepo wa maboma ya madarasa.”

Aidha ameongeza kuwa maboma ya nyumba za walimu yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kukaa muda mrefu bila kukamilishwa huku kukiwa na uhitaji mkubwa wa madarasa kutokana na ongezeko kubwa la watoto na kwamba kilio kikubwa cha wanafunzi wapatao 26,000 kilikuwa ni kukosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka juzi na mwaka jana.

Hata hivyo amefafanua uwepo wa kilio kikubwa cha maji hasa hasa vijijini kwa wakati huo, na kwamab hali hiyo ilikuwa ikiathiri shughuli za maendeleo na kutoa mfano kuwa “Walimu na watoto kufuata maji maeneo ya mbali na kukosekana kwa mahitaji ya maji katika maeneo muhimu kama Hosipitalini.”

Uingereza 'yakuna kichwa' mgogoro wa kiuchumi
Rais Mwinyi 'ateta' na Balozi wa Australia