Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Nchemba Amesema Serikali itaingiza zaidi Tsh 5 Trilioni Kwenye Mzunguko wa Fedha Hatua hiyo itawafanya Wananchi Kutosikia Machungu ya Tozo Mpya za Uzalendo Kwenye Miamala ya Simu.

Akizungumza Katika Uzinduzi wa Benki ya Biashara (TCB BANK) Dr Mwigulu Amesema Tozo Mpya za Miamala ya Simu zitaonekana Changamoto mwanzo lakini Mzunguko wa Fedha ukiongezeka na Fedha zikawa zinafikia Watu kwa Haraka Changamoto hiyo itaisha na Wananchi watazoea.

“Tumejipanga kuhakikisha tunatoa Fedha ya kutosha kwa Watoa huduma wa Serikali, Ikienda hivyo tulivyopanga tumedhamiria kutoa sio chini ya Tsh Trilioni 1 kwaajili ya Madeni tunayodaiwa na wazabuni wa Ndani ili kuibua wale Ambao Shughuli zao zilianza kupoa kwa Kuwa Fedha zimeshikiliwa Serikalini” Waziri Mwigulu Nchemba

Chanzo: Mwananchi

Mwakelebela: Sare zimetukosesha ubingwa
Mwalimu Mkuu Kortini kwa kughushi vyeti