Taasisi ya  Trade Mark East Africa (TMEA) imetoa msaada wa dolla za Marekani milioni 61 (shil. bilioni 132) za Tanzania  kwa Mamlaka ya Bandari(TPA) kwaaajili ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali ya Bandari ya Dar es salaam pamoja kuimarisha maeneo ya kuhifadhia makasha.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA, John Ulanga wakati wa kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam kati ya Mkurugenzi wa TPA, Deusdedit Kakoko na Mkurugeni Mkazi wa TMEA, John Ulanga, mradi huo utaanza kutekelezwa rasmi Januari mwakani na kukamilika mwaka 2019.

Aidha, Ulanga amesema msaada huo utaboresha na kupanua kina cha bandari ili kuwezesha meli zenye uzito mkubwa kuweza kutia nanga bandarini hapo” Itawezesha kuwepo kwa marekebisho balimbali ya miundo mbinu ili kuongeza ufanisi katika shughuli za upitishaji mizigo bandrini hapo.”amesema Ulanga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA Deusdedit Kakoko, amesema kuwa asilimia 90 hadi 95 ya mizigo hupitishwa bandarini hapo kwa mwaka na kwamba msaada huo utawezesha  meli zenye ukubwa  na upana wa mita 255 .

“TPA kwa sasa inapokea meli zenye uzito wa tani milioni 15 na baada ya maboeresho hayo itakuwa na uwezo wa kupokea meli zenye uzito wa tani milioni 26″alisema Kakoko.

“Lipumba ni mtu wa CCM…”
Waziri awasha moto TASAF, atumbua maofisa waandamizi wa mfuko huo