Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini ( TPDC), linatarajia kuongeza vituo 10 hadi 20 kwa jiji la Dar es salaam -Mtwara na Lindi, vya kujaza gesi asilia kwenye magari yaliyowekewa mfumo huo ambapo kipo kituo kimoja tu cha Ubungo kwa miaka kumi sasa ambacho hakikidhi mahitaji.
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC), Kapuulya Musomba alipotembelea maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea viwanja vya Sabasaba, Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani, ambapo amesema kuwa mwamko wa watumiaji upo vizuri tatizo hakuna vituo mikoani.
 
Amesema kuwa ili kufikia malengo yake ya kuongeza vituo vingi katika maeneo mbalimbali limejipanga kuruhusu na kukubaliana na watu binafsi wenye vituo vya mafuta kuweka gesi kwenye vituo vyao.
 
Aidha, ameongeza kuwa wataanza kuongeza vituo viwili ama vitatu Dar es salaam na kuendelea maeneo mengine, na kusema watatangaza tenda ili wawekezaji na watu binafsi wajitokeze kufanikisha hilo.
 
“Gesi asilia ikitumika kwenye magari inaweza kupunguza zaidi ya nusu ya gharama za mafuta na kuleta unafuu katika sekta ya usafirishaji nchini, wadau washirikiane nasi kwa kupata ufafanuzi EWURA na TPDC ili kufanya makubaliano,”amesema Musomba.
 
  • Majaliwa atoa agizo kuhusu eneo la Kata ya Kiomoni
  • Zitto aitwa polisi Kigoma
  • JPM afanya uteuzi
 
Hata hivyo alitaja mpango mwingine ni kuona wananchi wanafaidika na rasilimali ya gesi lakini wanakwenda kwa awamu kulingana na fedha wanayoipata.

RC Mwanri aunguruma jijini Dar, asema hata jirani 'Sukuma ndani'
Edinson Cavani kinara wa Golden Foot 2018