Katika kuhakikisha kuwa Gesi asilia inawafikia wananchi ili waweze kunufaika nayo, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeyataka Makampuni binafsi kuchangamkia fursa ya kushika Tenda katika mradi wa usambazaji wa gesi hiyo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.

Musomba amesema kuwa Shirika hilo limeanzisha mfumo wa kushirikiana na Sekta binafsi ili kuweza kupata urahisi zaidi kusambaza gesi katika mikoa iliyoainishwa na kuongeza kuwa TPDC mpaka sasa imekaribisha zaidi ya Makampuni 9 ambayo yamekidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.

“Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” amesema Mhandisi Musomba.

Amesema kuwa ili kuweza kufanikisha usambazaji huo wa gesi katika mikoa tajwa, TPDC inakaribisha na kuhamasisha Makampuni na Sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu yatakapomalizika.

Hata hivyo, Mradi huo wa usambazji gesi unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia kuanzia nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na vituo vya kujazia gesi hiyo.

Rais Kenyatta Atoa Onyo Kuhusu Uchaguzi wa Kenya
Jinsi ya kutumia fedha kidogo kufanikisha makubwa katika hali ‘ngumu’