Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imesema baadhi ya waamuzi wanakosa ujasiri, kuwasiliana, mwendelezo na kutumia akili ya kuzaliwa wanapochezesha mechi mbalimbali hapa nchini na ofisi yake inawakumbusha ili mwamuzi awe bora ni lazima awe na vitu hivyo, imefahamika.

Akizungumza na Kamati ya Waamuzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo, alisema kumekuwa na malalamiko mengi kwa waamuzi lakini ikifuatiliwa inagundulika baadhi wanakosa sifa hizo alizozitaja.

“Mwamuzi ni kama hakimu au jaji, ni lazima kwanza uwe jasiri, na mwamuzi mzuri anapimwa kwa vitu kama hivyo.”

“Kuna baadhi ya waamuzi wamekariri penalti haitoki dakika ya 94, au dakika ya kwanza, huko ni kukosa ujasiri, penalti inatoka dakika yoyote ile hata dakika ya 97 na kadi nyekundu inatoka muda wowote ule na anaonyeshwa yoyote yule,” amesema Kasongo.

Kocha Nabi achimba mkwara Young Africans
Kenya: Ruto ateta na wateule wake kukabili makali ya maisha