Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Bodi ya Ligi Kuu ya Zambia (ZPLB), Joseph Chimpampwe leo Jumamosi (Oktoba 16), ametembelea ofisi za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ‘TPLB’ na kufanya kikao cha kazi.

Chimpampwe amefanya kikao hicho na mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ‘TPLB’ Almasi Kasongo chenye lengo la kushirikishana uzoefu baina ya pande hizo mbili.

Kikao hicho kilihusisha pia
Wakuu wa Idara mbalimbali za TPLB na viongozi wa ZPLB (makamu mwenyekiti na Meneja wa Ligi) ambao walishiriki kwa njia ya mtandao wa Zoom.

Mkwasa: Azam FC inaweza kufanya maajabu Misri
Mashabiki 1000 kushuhudia Galaxy Vs Simba SC