Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya utunzaji bora wa hesabu kwa taasisi za umma zilizoandaliwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka  2015 mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam.

Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA), Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).

“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Mndeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi kwa weledi na uwazi hivyo kupelekea kupata tuzo ya heshima.

 

TFF Kuchunguza Kifo Cha Mchezaji Wa Mbao FC
Video: Waziri ataja mikoa 10 kuhusu Saratani