Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wametoa maoni na mapendekezo kwa Kamati ya Kitaifa ya Uboreshaji wa Mitaala, kuhusu uboreshaji wa mitaala unaondelea kwa kuongeza kipengele cha kodi katika mitaala ya elimu.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada ya umuhimu wa kuingiza masuala juu ya elimu ya kodi katika mitaala ya elimu ngazi ya msingi na sekondari.

Amesema, “TRA inaamini kwamba kama kungekua na somo la kodi linalosomwa na wanafunzi wote katika shule za msingi na sekondari tungeweza kuwa na raia wanaoelewa kodi.”

TRA inaamini kwamba kama kungekua na somo la kodi linalosomwa na wanafunzi wote katika shule za msingi na sekondari ingeweza kuwa na raia wanaoelewa umuhimu kodi: Kayombo.

Kayombo ameongeza kuwa, TRA inakusanya kodi kutoka kwa walipa kodi ambao hawana ufahamu na hawajui umuhimu wa kulipa kodi, hivyo kama wanafunzi watafundishwa somo la kodi shuleni, itasaidia kupata raia wenye uelewa mpana kuhusu kodi na kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiyari.

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa kamati ya Uboreshaji wa Mitaala, Prof. Maboko, amewashukuru TRA kwa maoni na mapendekezo waliyoyatoa na kuahidi kuyafanyia kazi  katika maboresho ya mtaala wa elimu nchini yanayoendelea.

PAC watumia Treni kukagua ujenzi SGR
Prof. Mkumbo: Hoja ziandaliwe mchakato wa marekebisho Sheria ya Habari