Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata na kutaifisha boksi 41 za mvinyo na pombe kali zilizokutwa katika duka la jumla jijini Dodoma zikiwa hazina Stempu za Kodi.

Boksi hizo zenye thamani ya shilingi milioni tatu ambazo ni mali ya Anthony George, zimekamatwa na kutaifishwa wakati Kamishna Mkuu wa TRA. Charles Kichere akikagua matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) Jijini humo kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.

Kichere amesema kuwa ni wajibu wa muuzaji kuhakikisha kwamba, vinywaji vinavyostahili kuwekewa Stempu za Kodi vinakuwa na stempu hizo ili kuisaidia Mamlaka kutoza kodi stahiki.

“Inatakiwa Stempu za kodi ziwekwe kwenye mzigo kabla mzigo huo haujanunuliwa na wauzaji wa rejareja. hii itaisaidia TRA kukusanya kodi halali na hatimaye kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali,”amesema Kichere

Hata hivyo Kwa upande mwingine, Kamishna Mkuu Kichere ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea
kutoa risiti kila wanapofanya mauzo na wananchi kwa kuhakikisha wanadai risiti kila wanapofanya manunuzi mbalimbali.

Sheria mpya ‘kuwafunga’ wasiowatunza wazazi wao
TCRA yaongeza muda wa usajili