Kufuatia kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe aliyoitoa katika ibada aliyoifanya Disemba 25, 2017 akidai kwamba anapesa nyingi kuliko Serikali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iliamua kumchukulia hatua madhubuti na kumfanyia uchunguzi kubaini ukweli wa kauli hiyo.

Leo TRA, imetoa ripoti kamili juu ya uchunguzi huo uliofanyika ukiwa na lengo la kujiridhisha na kubaini mambo yafuatayo;

  1. Askofu Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yeyote ya fedha hapa nchini.
  2. Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu akaunti za kanisa lake, zilizofunguliwa katika benki ya NBC, na kubainika kuwa akaunti hiyo ina jumla ya shilingi Bilioni 8 za Kitanzania, ambapo fedha hizo zinatokana na sadaka, zaka na michango mablimbali inayotolewa na waumini wa kanisa hilo.
  3. Kanisa la Askofu Kakobe limewahi kukwepa kodi ya shilingi milioni 20, ambazo zilitokana na uwekezaji katika kampuni ya kuuza mitaji.
  4. kampuni inayomilikiwa na watoto wa Kakobe imewahi kukwepa kodi ya shilingi milioni 37
  5. Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye majaba na mandoo kinyume na sheria ya utunzaji wa fedha na kipindi cha uchukuaji wa fedha hizo kanisa halizingatii maswala ya usalama kutokana na fedha nyingi zinazotolewa katika akaunti hiyo.
  6. Kanisa halina taratibu za kuandaa kitabu cha mahesabu ya mapato na matumzi kinyume na katiba ya kanisa pamoja na sheria za usimamizi wa pesa, hali inayopelekea fedha za waumini kutumika vibaya.
  7. Matumizi mabaya ya fedha yakiwemo Familia ya Kakobe pekee kufanya safari za nje ya nchi kwa kutumia pesa za waumini, pia Kakobe kutumia pesa za waumini kujenga nyumba ya mke wake yenye jina la mkewe ikimaanisha kuwa nyumba hiyo si mali ya kanisa, hali ambayo ni kinyume cha sheria.
  8. Pia wamebaini kuwa kupitia uchunguzi huo, wameweza kukusanya malimbikizi ya kodi ambazo zilikwepa kulipa jumla ya shilingi milioni 58 za Kitanzania.

 

Aidha mnamo January 24, 2018 Askofu Kakobe aliomba radhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kutokana na kauli zake za kebei pamoja na matamshi yake ya dharau akidai kuwa anapesa nyingi kuliko Serikali.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa wito kwa Taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki kwa wakati kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za kodi, Pia kufuata katiba zao ikiwa ni pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi kuonesha namna ambavyo pesa zinatumika.

Familia ya Akwilina yawasilisha bajeti ya mazishi ya binti yao.
Mambosasa aagiza vigogo 7 wa Chadema kuwekwa chini ya ulinzi