TRA kupitia kwa Kamishina Mkuu wa Ofisi hiyo wamezindua zoezi maalumu kwaajili ya kuhakiki na kuboresha  taarifa za usajili  wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN) .

Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Mkuu wa Ofisi hiyo Bw, Alphayo Kidata kwa kushirikiana na wafanyakazi wa ofisi hiyo mapema hii leo jijini Dar es salaam, hivyo kuanzia sasa zoezi hilo litakuwa endelevu katika mikoa yote nchini ya bara na visiwani .

Kidata alisema kuwa lengo kubwa la uzinduzi wa zoezi hilo ni kubadili mfumo wa sasa wa kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi kwa kuweka mfumo mpya unaoendana na ukuaji wa teknolojia ambao utakuwa na walipa kodi wake  wanaostahili kuwepo kwenye wigo.

Aidha aliongeza kuwa mfumo huo utasaidia  kuwaondoa walipa kodi hewa ,kuongeza ufanisi  katika suala zima la usimamizi wa ukusanyaji  kodi kwa kiwango cha juu na kuwezesha ulipaji kodi  kuwa nafuu kwa mlipaji.

Hata hivyo katika hatua nyingine Kidata ametoa wito kwa yeyote mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi kufika  katika ofisi za mamlaka hiyo ili kuweza kupata utaratibu wa zoezi zima  jinsi linavyokwenda

Tfda Yatoa Hundi Ya Milioni 17.7 Kwaajili Ya Madawati
Chadema Kilimanjaro watamba kushiriki Oparesheni Ukuta