Mabehewa sita ya Treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora  mpaka Dar es salaam, yameanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, ACP. Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi linaendelea  kufuatilia kutokana na  abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete, kwa ajili ya matibabu.

Aidha amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.

Mbaroni kwa kucheza muziki Msikitini
FC Bayern Munich yasajili watatu kwa MPIGO