Treni ya abiria inayofanya safari zake kati ya Stesheni na Pugu jijini Dar es salaam imepata ajali asubuhi ya leo Ijumaa ya Novemba 2, 2018 na kujeruhi watu tisa huku mabehewa mawili yakiharibika vibaya.

Kamanda wa reli Tanzania, David Mnyambugha amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo amesema kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Karakata lililopo wilayani Ilala.

“Ni kweli ajali imetokea leo asubuhi na kuna majeruhi tisa ambao wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu. Kuna mabehewa mawili ambayo hayafai kuendelea na safari hadi yavutwe,” amesema Mnyambuga.

Aidha, amesema taarifa za treni hiyo kama itaweza kuendelea na safari zake itaelezwa na wahusika ambao ni Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Malcom aahidi makubwa FC Barcelona
Mpanda kuanzisha bucha la kuuza nyama ya viboko

Comments

comments