Timu ya taifa ya Marekani, imeshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia ikitokea ukanda wa Amerika ya kati na kaskazini, kufuatia kufungwa na Trinidad na Tobago leo alfajiri.

Kikosi cha Marekani kilistahili kupata ushindi katika mchezo huo, ili kujihakikishia nafasi ya kwenda nchini Urusi, lakini kichapo cha mabao mawili kwa moja kilifuta ndoto za taifa hilo kubwa duniani.

Endapo Marekani wangepata ushindi wangefikisha point 15, ambazo zingewapeleka kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi na Amerika ya kati na kaskazini, lakini kufungwa kwao kumewafanya wamalize michezo ya kuwania kufuzu fainali za 2018 wakiwa kwenye nafasi ya nne kwa kufikisha point 12.

Hata hivyo Trinidad na Tobago hawakua na nafasi yoyote ya kufuzu fainali za kombe la dunia za 2018 kabla ya mchezo wao dhidi ya Marekani, na matokeo waliyoyapata yamechukuliwa kama sehemu ya kuwaharibia wapinzani wao.

Trinidad na Tobago imemaliza mkiani mwa msimako wa kundi la Amerika ya kati na kaskazini ilitanguliwa na timu za Marekani, Honduras, Panama, Costa Rica na Mexico.

Mshindi wa kwanza hadi watatu katika ukanda huo hupata tiketi ya kushiriki moja kwa moja fainali za kombe la dunia, huku aliyeshika nafasi ya nne hucheza mchezo wa mtoano dhidi ya mshindi Play Off kutoka Asia.

Ureno, Ufaransa zafuzu kombe la dunia, Marekani yatupwa nje
Mtuhumiwa hatari wa uhalifu auwawa

Comments

comments