Rais wa Marekani, Donald Trump amewataka Magavana nchini humo kufungua makanisa, misikiti na masinagogi, kwa kusema ni huduma muhimu.

Akitoa agizo hilo amewataka Magavana kuchukua uamuzi sahihi na kuruhusu sehemu za ibada kufunguliwa mara moja kwani Marekani inahitaji maombi zaidi.

Amesema baadhi ya Magavana wamefungua maduka ya vilevi na kliniki za kutoa mimba lakini wameacha sehemu za ibada, jambo ambalo amedai sio sahihi hivyo anasahihisha kosa hilo kwa kufanya ibada kuwa huduma muhimu.

Hata hivyo, kauli yake imeacha sintofahamu kwakuwa Serikali haina mamlaka ya kikatiba kuamuru majimbo binafsi kufungua biashara, makanisa au Shule.

Lindi: Madiwani sita wa upinzani wahamia CCM
Dubai kufunga biashara miezi 6 kutokana na Covid 19