Rais wa Marekani Donald Trump, ameanza kufanyia kazi ahadi zake ikiwemo kubadili sheria mbalimbali zilizokuwa zimepitishwa na rais mstaafu na aliyepita Barack Obama.

Aidha,Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa kwake Trump, ametoa amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei nafuu inayofahamika kama Obamacare, ambayo Trump aliahidi kufanyia marekebisho.

Trump pia amewaidhinisha mawaziri wake wapya wa Ulinzi na usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la seneti.

Utawala wa Trump umeanza kufanyia marekebisho mtandao wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa kipaumbele na uongozi huo mpya

Hata hivyo, utawala huo mpya unatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kuzifanyia kazi ahadi za Rais huyo Donald Trump, ikiwemo kutekeleza sera yake ya kuifanya Marekani kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani na kutekeleza sera ya Marekani kwanza.

Video: Possi - Nitajiuzulu ubunge, Mjadala kupanguliwa mawaziri washika kasi
Lipumba awananga Chadema,asema ni waroho wa madaraka