Donald Trump ameanzisha tovuti yake ya mawasiliano kwa lengo la kuchapisha taarifa moja kwa moja kutoka mezani kwake.

Kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Trump zilifungwa kwa madai alichochea vurugu zilizotokea Januari 6 katika Jengo la Bunge.


Tovuti ya Trump inakuja saa chache kabla ya uamuzi wa Bodi ya Facebook kutangaza ikiwa akaunti yake itafungwa moja kwa moja au la.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo, Mei 05, 2021.

Youtube inaangalia hali na itarudisha akaunti yake ikiwa itajiridhisha hakuna tishio la kweli la kuchochea vurugu. 

Twitter imemfungia moja kwa moja Trump aliyekuwa na wafuasi Milioni 88.

Niyonzima: Dakika 90 zitaamua
Mahakama yaifuta kesi ya Mdee na wenzake