Rais wa Marekani, Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya ghafla ya krismasi ya kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

Walisafiri kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru wanajeshi hao kwa huduma yao, mafanikio na kujitolea kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani.

Aidha, ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi, Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump katika eneo hilo.

Marekani ina wanajeshi 5,000 nchini Iraq kuunga mkono serikali katika vita dhidi ya kundi la Islamic State.

Hata hivyo mkutano uliopangwa kati ya Trump na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ulifutwa, huku ofisi ya Mahdi ikitoa sababu kubwa ni kutokubaliana na jinsi mkutano huo jinsi ungefanyika.

Mashindano ya Miss na Mr Albino Afrika Mashariki yalivyofana
SSRA kukibeba kikokotoo cha 25% nyumba kwa nyumba