Hatimaye jopo la wajumbe wa Majimbo ya Uchaguzi nchini Marekani limemuidhinisha rasmi Donald Trump kuwa Rais Mteule wa taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani akisubiri kukabidhiwa rasmi ufunguo wa ‘White House’, Januari 20 Mwakani.

Trump amepata ushindi wa zaidi ya kura 304 ya wajumbe, ambao kwa kawaida hufanya kazi rahisi ya kuidhinisha jina la mshindi wa uchaguzi wa urais kustahili kuwa Rais halali wa taifa hilo.

Wajumbe hao awali walipata ushawishi mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwataka kutompitisha Trump lakini ushawishi huo haukufaulu.

Baada ya kuidhinishwa rasmi, mfanyabiashara huyo mkubwa aliahidi kuanza na kazi ya kuwaunganisha Wamarekani wote na kwamba atakuwa rais wa wamarekani wote.

“Tumefanikisha! Asante kwa wote walioniunga mkono, tumeshinda rasmi uchaguzi (mbali na upotoshwaji na uvurugaji wa vyombo vya habari),” Trump ametweet.

Matokeo rasmi ya kura hizo za wajumbe yanatarajiwa kuwasilishwa rasmi mbele ya Bunge la Congress, Januari 6 mwakani.

Azam FC Waanza Kuiwinda Majimaji, Kuifuata Kesho
Young Africans Watoa Kauli Kuhusu Mgomo Wa Wachezaji