Rais wa Marekani, Donald Trump amesema hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni inayoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Nchini Marekani wanaoripoti matukio ya Ikulu

Trump ameyasema hayo ikiwa ni siku moja tu kupita baada ya kuwatuhumu vikali wanahabari kwa kuwataja kuwa ni adui wa watu kwa kudai wanaeneza taarifa za uongo na za kupotosha. Rais huyo mpya wa Marekani pia amewataja wanahabari kuwa ni wa Chama cha Upinzani Nchini Marekani.

Dhifa hiyo ilianzishwa mwaka 1921, huwa inahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu, wanasiasa wa Marekani, marais wastaafu na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wanavyofanyia kazi.

Rais wa Chama Cha Waandishi wa Habari wa Ikulu ya White House WHCA Jeff Mason amesema dhifa hiyo itaendelea kama ilivyopangwa kwani ni desturi ya kusherehekea mchango muhimu unaotekelezwa na mashirika ya habari katika taifa lililo huru.

Aidha ameongeza kuwa, sherehe hizo hufanyika kwa uhuru kwa kuangazia mafanikio ya uandishi habari katika ulingo wa kisiasa na kuwatambua wanafunzi bora wanaosomea uandishi ambao wanawakilisha kizazi kijacho cha tasnia hiyo ya habari.

DC Hapi aagiza Jeshi la Polisi kumuweka ndani Afisa uthamini wa Kinondoni
Gali la Mbunge laua, yeye anusurika