Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Donald Trump, kwa mara ya kwanza ameitakia mafanikio serikali mpya ya Rais Mteule Joe Biden anayetarajiwa kuapishwa baadaye hii leo.

Trump ambaye hajaonekana hadharani kwa wiki moja sasa, amevunja ukimya wake wa siku nyingi kupitia hotuba yake hiyo iliyorekodiwa kwenye mkanda wa video.

Trump kwa mara ya kwanza amewaomba Wamarekani kuiombea mafanikio serikali ijayo ya Biden, ikiwa ni mabadiliko ya msimamo wa wiki nyingi alizotumia kuishawishi idadi kubwa ya wafuasi wake wa Republican kuwa Mdemocrat huyo alifanya udanganyifu katika kinyang’anyiro cha urais.

Aidha, anatarajiwa kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Biden kama alivyotangaza juma moja lililopita, hii ikiwa ni mara kwanza kwa rais anayemaliza muda wake nchini humo kususia hafla ya uapisho wa rais mpya.

Tayari Rais mteule wa Marekani Joe Biden amewasili Washington katika mkesha wa sherehe ya kuapishwa kwake, baada ya kuagwa mjini Wilmington, Delaware, ambapo alitoa heshima kwa marehemu mwanawe wa kiume kabla ya kupanda ndege kuelekea katika mji mkuu.

David Alaba kukipiga Real Madrid
Wachambuzi wamchukiza Manara, atuma ujumbe Cameroon