Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa angalizo kwa nchi ya Venezuela kuwa itachukuliwa hatua kali endapo itaendelea na mpango wake wa kutaka kuibadili Katiba ya nchi hiyo ili iweze kumuongezea muda wa kutawala Rais wa sasa wa nchi hiyo Nicolas Maduro.

Kufuatia onyo hilo alilolitoa, Rais Trump pia ameupongeza upinzani nchini humo kutokana na kupigania kwake demokrasia na kumuelezea Rais Nicolas Maduro kama kiongozi mbaya ambaye anaota ndoto za kuwa dikteta.

Aidha, Vyama vya Upinzani nchini humo vimepanga kufanyika mgomo wa siku moja nchi nzima siku ya Alhamisi kama sehemu ya kampeni zake kupinga uamuzi huo wa Rais Maduro kubadili katiba.

Hata hivyo, wananchi wa nchi hiyo walijitokeza siku ya Jumapili kwaajili ya kupiga kura ya maoni isiyo rasmi kupinga pendekezo la kubadili katiba hiyo, lakini Serikali ikalipuuzia zoezi hilo la upigaji kura na kusema si halali.

Man United yaendeleza ubabe Marekani
Video: Chadema yatoa tamko zito, TRA yamkana Ngeleja Escrow

Comments

comments