Marekani imetangaza kuipatia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Serikali ya Marekani kupitia ofisi ya Rais Donald Trump imeeleza kuwa imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526 kutoka mfuko wa PEPFAR, ili kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi na virusi hivyo.

Mwakilishi wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser amesema kuwa wanalenga kufanikisha kizazi kilicho huru kutoka virusi nchini Tanzania. ”Kwa niaba ya raia wa Marekani, tunafurahia ushirikiano wetu na Tanzania na tunajitahidi kuhakikisha hakuna anyeachwa nje,” Amesema.

Ufadhili huo umelenga matibabu, ukaguzi, na kuzuia maambukizi mapya ya virusi hivyo kuanzia sasa hadi Septemba mwaka ujao, pia fedha hizo zitatumika kuimarisha maisha ya wajane na mayatima wa viurusi hivyo, kuzuia dhulma za kijinsia, pamoja na kuwafikia zaidi ya watu laki tatu walioambukizwa.

Aidha, Serikali ya Marekani itashirikiana na Serikali ya Tanzania kutekeleza huduma za kuwapima raia milioni 8.6 ili kuwawezesha kujua hali yao ya virusi, imeeleza taarifa hiyo ya BBC.

Fedha hizo zitapitia katika mashirika mbalimbali yanayoendesha miradi ya afya nchini Tanzania, kama vile (TACAIDS), na Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF)) yanatarajiwa kushiriki kufanikisha mpango huo.

Marekani ilikatiza ufadhili wake wa miradi kama hiyo nchini Kenya pamoja na kuyazuia mashirika dhidi ya kufanikisha miradi yoyote na wizara ya afya ya taifa hilo kutokana na usimamizi mbaya wa fedha.

Serengeti Boys Yaichapa Angola, Kombe la Dunia Lileee....!
Video: Serikali yazihamasisha Halmashauri kununua viuadudu nchini