Rais wa Marekani, Donald Trump ameitaka Urusi kujiandaa na shambulio la kombora litakalorushwa nchini Syria kujibu shambulio la kemikali lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji wa Douma.

Ameandika katika ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika kuwa Urusi inatakiwa kujiandaa kwa shambulio la kombora hilo litakalorushwa nchini humo.

Aidha, Maafisa wakuu wa Urusi wamesema kuwa wako tayari kujibu shambulio lolote litakalofanywa na Marekani nchini Syria.

Hata hivyo, Marekani na washirika wake ambao ni Ufaransa na Uingereza wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja na inasemekana wanajiandaa kutekeleza shambulio la kijeshi.

Naj amchoma Romy Jones kwa Baraka, ‘nataka uwe mchepuko’
Maharusi wafanya mtihani chuo kikuu dakika chache baada ya ndoa

Comments

comments