Raisi wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa yeye si mbaguzi na wala hana chembe chembe za ubaguzi mwilini mwake.

katika ukurasa wake wa kijamii, Trump ameandika kuwa ‘Mimi sio mbaguzi na wala sina chembe chembe ya ubaguzi mwilini mwangu;

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kushambuliwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii mara baada ya kutoa kauli ambayo iliashiria kuwabagua wabunge wanne wananawake ambao asili yao si nchi ya Marekani.

Katika ukurasa wake huo wa kijamii, yaani wa Twitter Trump aliwataka wanawake hao wasio na asili ya Marekani kuondoka nchini humo kurudi katika nchi walizotoka kama hawaridhishwi na hali ya usalama na amani nchini humo.

Kitendo hicho cha Trump kiliamsha ghadhabu na mijadala mbalimbali, kitu ambacho kilimfanya aibuke tena na kusema kuwa yeye hana chembe chembe zozote za ubaguzi mwilini mwake.

Aidha, bunge la wawakilishi linajiandaa kupiga kura ya makubaliano ya pamoja ya kukemea kauli zake, huku hatua hiyo ikitegemewa kupita kutokana na kuwepo wawakilishi wengi wa chama cha Democrats.

Awali, wabunge hao waliodai kubaguliwa na Trump, Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley na Rashida Tlaib waliutangazia umma kuyapuuza matamshi ya rais huyo wakidai yanalenga kuwaondoa kwenye mstari.

Wabunge hao wote wanne wamekuwa wakipambania suala zima la uboreshwaji wa huduma za afya, kupinga matumizi mabaya ya silaha, pia kushikiliwa kwa wahamiaji katika mpaka kati ya Marekani na Mexico wanasema ni masuala ambayo yanatakiwa kutizamwa kwa jicho la tatu.

Hata hivyo, Spika wa bunge kupitia tiketi ya chama cha Democratic Nancy Pelosi, ametangaza uamuzi wa kukemea matamshi hayo na amewataka wabunge wa Republican kuunga mkono azimio hilo.

BBC yafungasha virago nchini Burundi
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 17, 2019