Rais wa Marekani, Donald Trump ameonyesha ishara ya kulegeza misimamo yake ambayo amekuwa akiionyesha hadharani na kuisimamia kikamilifu mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Katika mazungumzo yao, Macron amesema kuwa anaheshimu sana uamuzi wa Trump wa kujitoa katika makubaliano ya tabia ya nchi wa Paris na kwamba Ufaransa itaendelea na juhudi zake kuhusu makubaliano hayo.

“Tuna tofauti zetu, Rais Trump ana ahadi za uchaguzi alizowapa raia wa taifa lake na pia mimi nilikuwa na ahadi, je vitu hivi vinapaswa kuturudisha nyuma katika maswala yote? Hapana, amesema Macron.

Aidha, kwa upande wake, Donald Trump amesema kuwa Marekani inaweza kubadili misimamo yake kuhusu mabadilko ya tabia ya nchi lakini hakutoa maelezo kwa kina kuhusu jambo hilo.

 

Rais huyo Marekani alijiondoa katika makubaliano hayo mwezi uliopita mwaka huu, huku akitaka kujadiliwa upya kwa makubaliano hayo ili kutoiingiza Marekani katika hatua isiyo na manufaa kwake kibiashara.

Hata hivyo, Macron amesema kuwa ni vyema kuweka kando makubaliano hayo huku viongozi hao wawili wakizungumza vile watakavyofanya kazi kuhusu maswala kama vile kusitishwa kwa mapigano nchini Syria na ushirikiano wa kibiashara.

 

 

Shughuli za mahakama zakwama nchini Uganda
Abidad, Modala wamuomba radhi Ommy Dimpoz kuhusu ‘Cheche’