Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amekitupia dongo kitengo cha Ujasusi cha Marekani kwa kushindwa kuanika mapema ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliompa ushindi mwaka jana.

Kupitia mtandao wa Twitter, Trump amedai kuwa kucheleshwa kutoa muhtasari wa uchunguzi uliofanywa na kitengo hicho kunatia mashaka kuwa huenda wanataka kupika kesi.

“Labda wahitaji muda wa zida ili kutengeneza kesi. Inashangaza sana,” aliandika Trump.

Hata hivyo, kitengo cha Ujasusi cha nchi hiyo kimetoa tamko kukanusha madai ya Trump kikieleza kuwa hakuna ucheleweshwaji wowote wa kutoa muhtasari huo kwa mujibu wa kalenda husika.

Vitengo vya usalama vya Marekani ikiwemo CIA na FBI vinaamini kuwa Urusi iliingilia moja kwa moja na kufanya udukuzi kwenye mfumo wa kielektroniki wa Marekani kwa lengo la kumharibia mgombea wa Democratic, Hillary Clinton na kumsaidia Trump (Republican).

Urusi imeendelea kukanusha vikali tuhuma hizo

Majaliwa akagua Maghala ya mahindi jijini Dar
Kinachojili kuhusu vitabu vya darasa la kwanza vyenye makosa chaanikwa