Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa nchi yake imekuwa ikishughulikia matatizo ya kibiashara baina  ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.

Amesema hayo katika mkutano wa nchi zenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani G7, ambapo amesisitiza kuwa Marekani na washirika wake wa Ulaya hukabiliwa na changamoto ndogo ndogo kidogo za biashara lakini pande zote mbili huwa zinafanya mazungumzo.

Amesema kuwa Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kipekee na anatumai watapata matokeo chanya kuhusiana na mvutano huo wa kibiashara uliojitokeza baada ya Marekani kuziongezea kodi bidhaa za chuma na bati za Umoja wa Ulaya.

Aidha, kwa upande wake, rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema kuwa mazungumzo yanayoendelea katika mkutano huo wa kilele wa G7 yanaonyesha dalili za pande zote husika kuwa na utayari wa kufikia makubaliano yatakayowanufaisha wote.

Hata hivyo, Trump aliwasili Canada kuhudhuria mkutano huo wa G7 akiwa ameshikilia msimamo wake kuwa maamuzi aliyoyachukua kuhusiana na biashara kati ya nchi yake na nchi sita wanachama wa G7 yanafaa ili kuzilinda kampuni na biashara za Marekani dhidi ya ushindani usiofaa wa kibiashara.

Video: Mkuchika kula sahani moja na wanaokwamisha mafao
Paka awagharimu baada ya kuingia uwanjani