Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa shirika la ujasusi la nchi hiyo CIA halijahitimisha uchunguzi wake kwa kumlaumu Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman kwamba ameamuru mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Khashoggi aliuawa Oktoba 2 ndani ya ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki. ambapo wakati wa uhai wake alikuwa mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme bin Salman na alikimbilia Marekani mwaka 2017 akihofia usalama wake.

Aidha, maafisa wa CIA waliviambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa operesheni ya kumuua Khashoggi iliamuriwa na bin Salman

.

Mamlaka za Saudia Arabia zimesisitiza kuwa operesheni hiyo ilikuwa haramu na bin Salman hakuwa na ufahamu wowote wa kutokea kwa mauji hayo.

Kauli hiyo ya Trump ameitoa wakati ambapo bin Salman ameanza ziara ya kikazi nje ya nchi yake toka Khashoggi alipouawa. kwasasa yupo katika nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo ni mshirika mkubwa wa Saudia ndani ya kanda ya Mashariki ya Kati.

“CIA wanahisia mbalimbali. ninayo ripoti yao, na hawajahitimisha, na sijui kama kuna mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kuwa mwanamfalme (bin Salman) kuamuru mauaji,”amesema Trump

Hata hivyo, Trump amekuwa mstari wa mbele kusema kuwa Saudia ni mshirika mkubwa wa Marekani, na asingetaka kuharibu uchumi wa dunia kwa kuwawekea vikwazo kutokana na mauaji hayo.

Wakazi wa kanda ya ziwa watakiwa kuchangamkia fursa
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 23, 2018

Comments

comments