Rais wa Marekani, Donald Trump amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na mtu mmoja kwa kutumia bomu la jadi, katika tamasha la muziki jijini Manchester nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo na kuua watu 22 na wengine 60 kujeruhiwa.

Trump ambaye aliapa kupambana na ugaidi kwa nguvu zote, amesema kuwa washambuliaji hao ni waovu walioshindwa.

“Sitaki kuwaita kuwa ni wanyama kwa sababu wanaweza kupenda hilo neno. Nitawaita ‘waovu walioshindwa,” alisema Trump kwenye hotuba yake aliyoitoa mjini Bethlehem.

Kutokana na tukio hilo, watu wengi wameendelea kutumia mitandao ya kijamii kuwatafuta ndugu na jamaa ambao walikuwa kwenye tamasha hilo.

Viongozi mbalimbali wa dunia wameendelea kutuma salamu zao za rambirambi na kuonesha jinsi walivyoguswa na tukio hilo, lilitokea kwenye tamasha la mwanamuziki wa kike, Ariana Grande.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ambaye pia alitoa pole zake, amepanga kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May. Ufaransa pia ilipata pigo la kigaidi Novemba mwaka juzi, shambulizi ambalo lilifanyika kwenye tamasha la muziki.

Mwanri apiga marufuku usafishaji tumbaku Tabora
Aliyekuwa Rais wa Korea Kusini Afikishwa Mahakamani, Pingu Mikononi