Rais wa Marekani, Donald Trump amekana tuhuma za kuhusika kwake katika kutumia fedha za kampeni wakati wa mikutano ya kampeni kuwalipa wanawake wawili ambao wanasadikiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Katika kesi iliyosikilizwa hivi karibuni katika mahakama iliyopo New York mapema wiki hii , mwanasheria wa zamani wa rais Trump, Michael Cohen amesema kuwa Trump alimpa maelekezo kutoa fedha kwa lengo kuu la kuwashawishi wanawake hao kukaa kimya wakati wa uchaguzi wa rais wa mwaka 2016.

Aidha, rais Trump amekuwa akimshutumu mwanasheria huyo kwa kupika mambo dhidi yake kwa lengo la kupata huruma ili kuepuka kifungo.

Hata hivyo, Ikulu ya Marekani imesisitiza kuwa kuvunja sheria ya fedha za kampeni kwa Michael Cohen haimaanishi kuwa Rais trump naye atawajibika,

Malipo yeyote kama yakifanyika kwa siri kwa niaba ya mwanasiasa ama mgombea yeyote yanaweza kuchukuliwa kama ukiukwaji wa sheria za kampeni nchini Marekani

 

Video: Lugola azidi kuibana polisi, Watu 700 wa virusi vya ukimwi watoweka
Cristiano Ronaldo afichua siri ya kuihama Real Madrid