Rais wa Marekani, Donald Trump amemkosoa vikali aliyekuwa muigizaji wa ‘Empire’, Jussie Smollet na kesi aliyoifungua Chicago akidai kushambuliwa na watu waliokuwa wafuasi wa rais huyo.

Rais Trump ambaye yuko Japan kwa ajili ya kukutana na kiongozi mpya wa nchi hiyo, ameeleza kupitia Twitter kuwa Smollet ambaye alitaka kutumia msemo wa ‘Make America Great Again (MAGA)’ kujidai ameshambuliwa na wafuasi wake, aliwakosea wafuasi hao.

Muigizaji huyo aliwahi kushtaki polisi akidai kuwa alivamiwa na watu wawili usiku akiwa anatembea mtaani na kwamba mmoja alipaza sauti akisema ‘Hii ni nchi ya MAGA’.

Hata hivyo, muigizaji huyo alituhumiwa baadaye kwa kufungua kesi ya uongo na kwamba watu wawili walioonekana wakimvamia aliwatayarisha mwenyewe na kuwalipa kufanya hivyo. Kesi dhidi yake ilifutwa baadaye.

“Kwa ziada ya tatizo la kutokuwa wafanisi na rushwa, kesi ya Smollet akiwa Chicago ilikuwa ni kosa la chuki. Kumbuka, ‘[walisema nchi ya MAGA ndiyo’ lakini yote yakageuka kuwa uongo mkubwa. Ni vitu muhimu sana lakini hata hakuwaomba radhi mamilioni ya watu aliowadanganya!” tafsiri isiyo rasmi ya tweet ya Trump.

Hii sio mara ya kwanza Trump anazungumzia suala hilo, kwenye baadhi ya hotuba zake za hivi karibuni amewahi kuitaja Chicago kuwa sehemu ambayo kumekuwa na ongezeko la mashtaka ya uongo katika vituo vya polisi huku akitaja mfano wa kesi ya Smollet.

Mei 21, Trump aliandika tweet ambayo alimtaja Smollet akimhoji kuhusu mamilioni ya watu ambao aliwaudhi.

Kutokana na sakata hilo, waandaaji wa ‘Empire’ walimuondoa Smollet kwenye mradi huo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 27, 2019
Sugu afikiria namna ya kuacha muziki, ajiuliza maswali