Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha bajeti kubwa ya dola bilioni 400 baada ya kufikia makubaliano mapema ambayo yalikuwa na azma ya kuepusha kufungwa kwa shughuli za serikali kuu.

Rais Donald Trump amesaini makubaliano hayo katika Ikulu ya White House hii leo ili kuepusha kufungwa kwa shughuli za serikali kuu.

Aidha, fedha hizo zitatumika katika shughuli za serikali kuu mpaka Machi 23, ambapo Wabunge wamepewa muda wa kuandika kwa kina mpango wa matumizi kwa kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha ambao unamalizika Septemba 30.

Serikali ya Marekani ilifungwa Ijumaa asubuhi wakati bunge lililposhindwa kufikia muafaka katika muda wa mwisho ili kupitisha bajeti ya kuifadhili tena serikali kuu. Ufungaji wa baadhi ya shughuli za serikali kuu ulikuwa wa pili ndani  kipindi cha mwezi mmoja.

Hata hivyo, Bajeti ilipitishwa licha ya baadhi ya wanasiasa wapinzani kupinga ongezeko kubwa katika matumizi, na bila ya mpango wowote wa kuchukua hatua za kuwalinda wahamiaji vijana zaidi ya milioni moja ambao hawana makaratasi halali, wanaojulikana kama “Dreamers.”

 

Rais Durtete abuni mwarobaini wa wakwepa kodi
Jaji Mutungi: Fuateni sheria ya gharama za uchaguzi

Comments

comments