Rais wa Marekani, Donald Trump amesaini Sheria inayoruhusu kuundwa kwa Kituo cha Kijeshi cha Angani na kuwapa wafanyakazi wa Serikali kuu wiki 12 za likizo ya Uzazi kwa Wazazi wote wawili.

Baraza la Seneti linalodhibitiwa na Republican limeidhinisha Muswada wa Sera ya Ulinzi yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 738 baada ya Baraza la Wawakilishi linalodhibitiwa na Democrat kupitisha uamuzi huo wiki iliyopita

Aidha hatua hiyo itawezesha kuanzishwa kwa Kituo cha Kijeshi cha Angani kilichopendekezwa na Trump ikiwa ni Tawi la sita la Jeshi la Marekani.

Jenerali John Raymond, Kamanda wa Kituo cha Kijeshi cha Angani (Space Command) na Kituo cha Jeshi la Anga (Airforce Space Command) ameita Tawi hilo jipya kuwa la muhimu kwa Taifa na kusema, Uongozi wa Marekani katika anga za juu utawavutia wengine ulimwenguni.

Polisi aliyekataa rushwa ya Sh10 milioni apandishwa cheo
Maiti yagoma kuzikwa kisa kulipiwa mahari