Mgombea urais wa chama cha Rupublican nchini Marekani Donald Trump amesema kuwa atabuni mfumo ambao utasaidia serikali yake kudhibiti uhamiaji kutoka nchi mbalimbali duniani.
Akizungumza wakati wa kampeni katika jimbo la Iowa Trump alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuwatimua watu wote ambao ni ving’ang’anizi nchini Marekani licha ya muda wa visa zao kumalizika.
Pia alikumbushia azmayake ya kujengwa ukuta kati ya mpaka wake na Mexico kuwazuia wahamiaji wanaotoka nchi mbalimbali kupitia nchi jirani.