Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais wa nchi hiyo, Donald Trump anaunga mkono juhudi za serikali kuimarisha uchunguzi dhidi ya wateja wanaotaka kununua silaha, ambapo amefikia hatua baada ya wiki iliyopita kutokea mauaji ya wanafunzi 17 kwenye shule ya sekondari ya Marjory Stoneman Douglas iliyoko Parkland jimbo la Florida.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo, Sarah Huckabee Sanders ambapo amesema kuwa Rais Trump alizungumza wiki iliyopita na seneta wa jimbo la Texas -Republican, John Cornyn kuhusu muswada wake unaoshirikisha vyama vyote kwamba kunahitajika kuboresha uchunguzi kwa wanunuaji bunduki.

Aidha, katika ripoti ya polisi kuhusu tukio lililotokea wiki iliyopita imesema kuwa, Nikolas Cruz mwenye umri wa miaka 19 aliwaua wanafunzi 14 na watu wazima watatu huko Parkland, Florida kwenye shule ya sekondari ambayo alisimamishwa masomo tangu mwaka jana.

Hata hivyo, Cruz amefikishwa mahakamani Jumatatu wakati mawakili wakijadili utaratibu wa kesi ya mauaji dhidi yake.

Wanafunzi wa kike wawatoroka Boko Haram shuleni
Makamu wa Rais atoa maagizo mkoani Simiyu