Rais wa Marekani, Donald Trump ametishia kuitoa Marekani katika Shirika la Biashara Duniani WTO iwapo shirika hilo litashindwa kubadilisha utendaji wake.

Rais Trump amekuwa akishinikiza sera zinazoitetea nchi yake akisema kuwa Marekani inaishughulikiwa isivyo sawa na shirika hilo.

Aidha, Shirika hilo la Biashara duniani lilianzishwa kwa ajili ya kusimamia sheria za biashara duniani na kutatua tofauti kati ya nchi na nchi.

Onyo lake hilo la kutaka kujitoa katika Umoja huo umeonyesha mvutano uliokuwepo kati ya sera za kibiashara za rais huyo na mfumo wa biashara huru ambao shirika hilo unasimamia.

Pia hivi karibuni Marekani ilipinga uchaguzi wa majaji wapya wa mfumo wa WTO wa kukabiliana na mashauri jambo ambalo linaweza kudhorotesha uwezo wa kutoa hukumu.

Hata hivyo, Mwakilishi wa Marekani katika masuala ya biashara Robert Lighthizer naye amekuwa akiinyoshea kidole WTO kwa kuingilia mamlaka ya Marekani.

 

Kanye West amwaga machozi akiomba radhi redioni
Sethi alia na kutowasiliana na mkewe

Comments

comments