Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong un hayatazaa matunda basi ataachana na mazungumzo hayo.

Katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, Trump na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe wamesema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti liendelee kwa kukataa kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Aidha, waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe yuko katika mgahawa wa rais Trump wa Mar-a-Lago resort mjini Florida kwa ajili ya mazungumzo.

Vile vile, Trump amethibitisha kwamba mkurugenzi wa CIA, Mike Pompeo alifanya ziara ya kisiri hadi Korea Kaskazini ili kukutana na Kim Jong Un.

Hata hivyo, kwa upande wake waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amemtaka rais Trump kusaidia kuachiwa huru kwa raia wa Japan waliotekwa nyara na Korea Kaskazini miaka ya 1970 na 1980.

Wauguzi 10,000 wafukuzwa kazi kwa kufanya mgomo
Video: Aliyejiita mtoto wa Lowassa Mbaroni, Zitto na Polepole wavaana...