Raisi wa Marekani, Donald Trump ametoa masharti mapya kwa raia wa nchi za Kiarabu kuingia nchini humo kwa shughuli mbalimbali.

Aidha, katika masharti aliyoyatoa, Trump amesema kuwa kila mtu atakayekuwa anasafiri kuelekea nchini humo ni lazima awe na mwenyeji wake wa Kimarekani.

Masharti hayo yamezilenga nchi za Iran, Libya, Somalia, Syria, Yemen na Sudan ambapo raia wake watatakiwa kuwa na ndugu zao nchini Marekani ama rafiki ili waweze kupata ruhusa ya kuingia nchini humo.

Hata hivyo, masharti hayo yamekuja mara baada ya Mahakama kuu nchini Marekani kuizinisha agizo la rais wa nchi hiyo ambalo lilikosolewa vikali kwa kuwazuia raia kutoka nchi za Kiislam kuingia nchini humo.

Antonio Conte Ashtuka, Azuia Uhamisho Wa Matic
Bafetimbi Gomis Atimkia Uturuki