Rais Donald Trump wa Marekani ameziita harakati za Saudi Arabia za kuficha ukweli juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi kuwa ni mbaya zaidi kuwahi kutokea na kwamba ni za kihistoria.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, -Trump amesema kuwa mtu yeyote aliyepanga mauaji hayo anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

“Walikuwa na wazo duni sana na wakalitekeleza vibaya mno, na kiufupi harakati zao za kuuminya ukweli ndio mbovu zaidi katika historia ya kujaribu kuficha ukweli”, ameongeza Rais Trump.

Marekani imekuwa ikipata shinikizo kutoka Uturuki pamoja na Jumuiya ya Kimataifa la kuwabana washirika wao Saudi Arabia kuhusu mauaji hayo ya Kashoggi yaliyotokea kwenye ofisi za ubalozi mdogo wa nchi hiyo jijini Instanbul, – Uturuki.

Baada ya Rais Trump kutoa kauli hiyo,  Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, –  Mike Pompeo ametangaza kufutwa hati za kusafiri za kuingia  nchini Marekani kwa  zaidi ya watu ishirini wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya mwandishi huyo wa habari.

Khashoggi anadaiwa kuingia kwenye ofisi hizo za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Instanbul, – Uturuki Oktoba pili mwaka huu kwa lengo la kushughulikia nyaraka binafsi na hakutoka tena.

Awali Saudia walisema kuwa alitoka  na baada ya shinikizo kubwa kutoka Uturuki pamoja na Jumuiya ya kimataifa ikakiri kuwa aliuawa alipojaribu kupambana na baadae ikasema kuwa Kashoggi ameuawa katika operesheni isiyo rasmi.

TOC yafafanua mipango ya kufuzu Olimpiki 2020
Trump, Putin kuteta jijini Paris

Comments

comments