Siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuapishwa kuwa kiongozi wa taifa hilo kubwa duniani,amevilaumu baadhi ya vyombo vya habari nchini humo baada ya kueneza taarifa za uongo juu ya idadi ya watu waliohudhuria katika sherehe ya kuapishwa kwake.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, White House, Sean Spicer, amesema kuwa vyombo hivyo vya habari vinaendesha kampeni ya kuwagawa wamarekani  kwa kutoa taarifa ambazo si sahihi na hazina msingi wowote.

Hata hivyo kanda za video za matangazo ya moja kwa moja wakati wa hafla hiyo hazikuweza kunasa umati mkubwa wa watu ambao Donald Trump anawasema kuwa walihudhuria katika sherehe hizo, takwimu zinaonyesha kuwa umati mkubwa ulihudhuria kwenye sherehe za kuapishwa kwa rais mstaafu Barack Obama mwaka 2009 kuliko za mwaka huu za kwa Trump kitu ambacho anakipinga.

Kwa upande wake Rais huyo wa Marekani amesema kuwa video na picha wakati wa kuapishwa kwake zilionyesha taarifa ziziso za ukweli.

“Walionekana kama watu milioni 1.5 siku ya Ijumaa wakati nikiapishwa, amesema Trump,wakati vyombo mbalimbali vya habari vililipoti kuwa watu walikuwa chini ya 250,000, na amewatuhumu waandishi wa habari kuwa ni waongo kuliko mtu yeyote duniani.

 

Video: Mwinyi awataka watanzania kuendelezo mambo mema
Jammeh kuanza maisha mapya Equatorial Guinea