Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa uvumilivu dhidi ya vitendo vya kijeshi vinavyofanywa na Korea Kaskazini umefika kikomo.

Akizungumza jana katika Ikulu ya Marekani akiwa na Rais wa Korea Kusini, Moon-Jae, Trump alisema kuwa nchi hizo mbili zitaendelea kuimarisha uhusiano kati yake na kuithibiti Korea Kaskazini.

Kipindi cha kendelea na uvumilivu kwa utawala wa Korea Kaskazini kimeshindwa. Hakika, uvumilivu huo umekwisha,” alisema Trump.

Aliongeza kuwa nia ya Marekani ni kuhakikisha kuna amani katika eneo hilo lakini pia itaendelea kujilinda dhidi ya vitendo viovu vya Korea Kaskazini, pamoja na kuwalinda washirika wake.

Naye Rais wa Korea Kusini alieleza kuwa nchi hizo zitashirikiana kujibu vitendo viovu kwa njia zote ikiwa ni pamoja na kuweka vikwazo zaidi huku akitoa nafasi pia kwa mazungumzo.

Kiongozi huyo wa Korea Kusini aliyemtembelea Trump, aliungana na wito wa Rais huyo wa Marekani kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.

Wakati hayo yakiendelea, Korea Kaskazini imeendelea kushikilia msimamo wake wa kufanya majaribio ya makombora ya kinyuklia, huku ikiongeza ubora zaidi wa makombora yake na kudai kuwa yanafika katika kona nyingi za dunia ikiwa ni pamoja na sehemu ya Marekani.

?Live: Kamati ya katiba na sheria bungeni yakutana kufanya marekebisho ya sheria
Young Killer Ampa Nay wa Mitego Masharti ili Waende Sawa