Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa mkutano wake na Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un hautafanyika mpaka pale kiongozi huyo atakapo timiza masharti yaliyopangwa.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Senders mara baada ya kupokea ombi la kufanya mazungumzo kutoka kwa Rais wa Korea Kaskazini.

Kukubali kwa Trump mwaliko wa Kim bila masharti hapo awali kulipokelewa kwa mshituko mkubwa na jumuiya ya kimataifa kwani hakuna rais wa Marekani aliyewahi kukutana na Rais wa Korea Kaskazini akiwa madarakani.

“Mkutano huu hautafanyika hadi pale tutakapoona masharti yaliyowekwa yanatimizwa na Korea Kaskazini,” amesema mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya Marekani Sarah Senders

Amesema kuwa Marekani haijafanya maridhiano yoyote na Korea kaskazini, wakati Korea kaskazini imetoa ahadi ya kuachana na mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia.

Hata hivyo, Rais Trump ana matumaini makubwa kwamba hatua zaidi zinaweza kuchukuliwa na Korea Kaskazini kuhusu kusitisha mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia.

 

Video: Watakao andamana watasimulia- JPM, Maandamano ya Mange Kimambi yaleta hofu mpya
Jeshi la polisi: Msifuate mkumbo kuandamana