Rais wa Marekani, Donald Trump ameamua kuwa tembo asiyezuilika kunywa maji kwa kelele, akionekana kutojali maandamano makubwa yanayoendelea dhidi ya ziara yake barani Ulaya, na sasa amepanga kucheza golf wakati maandamano yakiendelea.

Trump ambaye jana jioni aliingia nchini Scotland baada ya kukamilisha ziara yake nchini Uingereza alikokabiliwa na maandamano makubwa, anakabiliwa na maandamano makubwa zaidi katika nchi hiyo leo, yakiitwa maandamano ya kitaifa.

Hata hivyo, Rais huyo wa Marekani amepanga kucheza golf kwenye hotel yake ya kifahari iliyoko Ayrshire, wakati maandamano hayo yakiwa yanaendelea.

Maandamano hayo ya kitaifa yatakayovuta maelfu ya watu yatafanyika leo kuanzia kwenye eneo la bunge la Scotland kwa lengo la kupinga sera zake.

Trump ambaye mama yake mzazi alikuwa raia wa Scotland, ameingia nchini humo kwa mapumziko ya siku mbili akiwa na mkewe, Melania. Watapumzika kwenye hotel yake iitwayo Turnberry.

Maelfu waliandamana jijini London Ijumaa, kupinga ziara ya Trump nchini Uingereza. Ingawa kulikuwa na maandamano hayo, Rais huyo wa Marekani alikutana na Waziri Mkuu na wote kwa pamoja walizungumza na waandishi wa habari.

 

Ziara hiyo, pamoja na changamoto zake, itaimarisha zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili ambazo ni washirika wakuu.

Mugabe amuahidi mpinzani mabilioni, magari kuendeshea kampeni
Video: Wanawake 800 waomba kuolewa na tajiri Dangote, Maajabu matokeo ya kidato cha sita

Comments

comments