Rais wa Marekani, Donald Trump leo amezindua rasmi mkakati wake wa kampeni ya mwaka 2020, akiomba kupewa ridhaa ya kuliongoza Taifa hilo kwa muhula wa pili.

Rais huyo kutoka Chama Cha Republican ametangaza nia yake mbele ya maelfu ya wafuasi wake katika Jimbo la Florida, akiwataka kumpa nafasi nyingine ya miaka minne.

Katika tukio hilo, alirusha makombora kwa chama cha Democratic akidai kuwa ni chama ambacho kinataka kuliharibu Taifa hilo lenye nguvu.

Mke wa Rais Trump, Melania alimuunga mkono mumewe akieleza kuwa ana furaha kuu na angependa kuendelea kuwa mke wa Rais kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka Ikulu ya Marekani akiwemo Makamu wa Rais, Mike Pence ambaye pia alizungumza.

Katika hotuba yake iliyokuwa na dakika 80, Rais Trump alikumbushia mambo muhimu yaliyosababisha kushinda uchaguzi 2016.

Rais Trump aliahidi kuendelea kuhakikisha anapambana na wahamiaji haramu ikiwa ni siku moja baada ya kueleza kupitia Twitter kuwa chombo maalum alichokiunda kitaanza kazi punde kuhakikisha inawaondoa nchini humo mamilioni ya wahamiaji haramu.

Merkel aikomalia Iran kuhusu mashambulizi ya meli
Tusiwanyanyase Wafanyabiashara hawa- IGP Sirro