Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Korea kaskazini, Kim Jong Un wamekutana na kufanya mazungumzo katika eneo lisilo na shughuli za kijeshi linalozitenganisha Korea kaskazini na Korea Kusini, Panmunjom.

Trump aliwasili Seoul Korea Kusini jana Jumamosi kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo, Moon Jae-in baada ya kuhudhuria mkutano G-20 nchini Japan.

Hii ni mara ya tatu katika muda wa miezi 16 tangu mkutano wao wa kilele wa pili kuvunjika nchini Vietnam waliposhindwa kusuluhisha tofauti na misimamo mikali kati yao.

Marekani yaanza mazungumzo na Wanamgambo wa Taliban
Kibiti yahusishwa mauaji ya Watanzania 9 Msumbiji, Sirro atuma salamu kwa Wauaji