Hatimaye, Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili leo nchini Singapore kwa ajili ya kufanya mkutano wao wa kihistoria.

Kim alikuwa wa kwanza kutua nchini humo, takribani saa saba kabla ya Trump kutua akiwa ndani ya ndege maalumm ya Air Force One.

Mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo utafanyika Jumanne ijayo katika hotel ya kifahari ya Sentosa, Kusini mwa Pwani ya Singapore.

Marekani imeendelea kuwa na matumaini kuwa baada ya mkutano huo, Korea Kaskazini itaanza kwa uhakika mchakato wa kuachana na mpango wake wa silaha za kinyuklia.

Aidha, kuwasili kwa Kim Jong Un uliwachanganya waandishi wa habari na wachambuzi wa maeneo mbalimbali duniani waliopo nchini  Singapore kuripoti tukio hilo la kihistoria, wasijue kwa uhakika ni ndege na gari lipi iliyombeba kiongozi huyo pamoja na hoteli aliyofikia. Hii ni tofauti na ilivyokuwa kwa Trump ambaye kuonekana kwa Air Force One angani kulijieleza.

Wakiwa makini kuripoti ujio huo, kwanza ilitua ndege ya illyushin. Hiyo ilikuwa rahisi kuitambua kwani ni ndege ya ulinzi binafsi ya Kim Jong Un yenye silaha maalum ambayo hutangulia.

Kisha ilishuka ndege ya Air China 747 ambayo humbeba rais wa China, Xi Jinping. Wanahabari wengi waliripoti moja kwa moja kuwa wanaamini Kim yuko ndani ya ndege hiyo.

Lakini ghafla ilishuka ndege nyingine ambayo ni ndege binafsi ya Kim Jong-un, dege la Ki-Soviet aina ya Ilyushin Il-62, ambayo pia walihisi ndiyo aliyokuwamo kiongozi huyo.

Gari aina na Mercedes ambayo wengi waliamini amepanda ilionekana ikishusha watu wote lakini kiongozi huyo pia hakuwemo! Bila kutarajiwa, aliwasili akiwa katika gari aina ya Mercedes-Maybach.

Singapore inakuwa nchi ya kwanza ya mbali ambayo Kim ameitembelea tangu alipoingia madarakani mwaka 2011. Safari yake ya kwanza nje ya nchi ilikuwa China na Aprili alikuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kukanyaga ardhi ya Korea Kusini, alipokutana na Rais Moon Jae-in kwenye mpaka wan chi hizo.

Magazeti ya Tanzania leo Juni 11, 2018
Lil Wayne, Birdman wakunja makucha, wajipanga upya