Rais mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani masaa machache yajayo, mbele ya haraiki ya watu zaidi ya 750,000 katika makao makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C. huku Maandamano makubwa yakitarajiwa kufanyika sehemu mbalimbali duniani kwa makundi yanayompinga na yale yanayomuunga mkono, kwa Marekani maandamano hayo yatafanyika katika mji Mkuu wa nchi hiyo.

Wanawake pia wanatajwa kujipanga kufanya maandamano mjini Washington Jumamosi  na yanatarajiwa kuwa na umati wa watu zaidi laki mbili (200,000).

Vilevile Maandamano mengine ya aina hiyo pia yanatarajiwa kufanyika katika maeneo mbali mbali dunia ambapo waandamanaji watakusanyika katika miji  mbalimbali ikiwemo Brussels, Sydney na London leo na Kesho.

Mapema hii leo Ijumaa, Kikundi cha watu wenye itikadi za mlengo wa kushoto na wanaharakati wa kiislam wanaompinga Trump wamekuwa wameandamana nje ya ubalozi wa Marekani mjini Manilla-Ufilipino.

Kiongozi wa maandamano hayo Renato Reyes ameliambia shirika la habari la AP kwamba Trump “ameonyesha aina ya sura ya ndani ya ukoloni unaovuka mipaka ” na kumtaka rais wa nchi hiyo Rodrigo Duterte kuendelea kuwa huru juu ya sera yake ya kigeni.

Hata hivyo, Trump kama ilivyo kawaida yake ya kuandika kwenye Twitter, teyari ameshaandika kuwa”Tukutane saa tano mchana kwenye sherehe ya kuapishwa kwangu” amesema Trump.

Aidha rais huyo mteule wa Marekani anatarajiwa kuapishwa  saa tano kamili asubuhi kwa saa za Marekani na Saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Trump wa chama cha Republican anapokea kijiti kutoka kwa Rais Barack Obama wa Chama cha Congress.

 

Live Washington: Sherehe za kuapishwa Donald Trump kuwa Rais Marekani
Exclusive! Dark Master aeleza maisha baada ya kifo cha Albert Mangweir na matumizi ya madawa ya kulevya.